Nyoka-miti ni nyoka wa jenasi Dipsadoboa katika familia Colubridae. Amepewa jina hili kwa sababu hukaa mitini takriban masaa yote.
Nyoka hawa ni warefu kiasi, m 1.4 kwa kipeo lakini sm 60-90 kwa kawaida. Rangi yao ni kijani au kahawia. Spishi kahawia zina kilingo kama marumaru. Rangi hizi zinaweza kuchukuliwa kama rangi za kamafleji.
Kama jina lao linadokeza huishi mitini ambapo hukamata vyura, mijusi-kafiri na vinyonga.
Chonge ni meno ya nyuma lakini sumu yao haina hatari kwa watu.