Beauveria ni jenasi ya kuvu entomopathojeni (kuvu zisababishazo magonjwa kwa wadudu) katika familia Cordycipitaceae. Kuvu hizi hazina jinsia na ni anamorfi za spishi za Cordyceps (teleomorfi zao). Spishi za Beauveria zinazaa spora nyeupe au njano ambazo ni ndogo sana na hazichanganyiki na maji. Zinazaliwa juu ya hife kwa umbo wa zigizaga.
Spishi za Beauveria huonekana sana zikimea juu ya mizoga ya wadudu. Zinatokea pia katika udongo kila mahali pa dunia, isipokuwa Antakitiki, na hata ndani ya mimea (endofiti). Spishi kadhaa, kama Beauveria bassiana na B. brongniartii, hutumika kama dawa za kibiolojia dhidi wadudu waharibifu.
Tangu kuwadia kwa mihtasari ya jenetiki imewezekana kutambua spishi zaidi kuliko zamani. B. bassiana na B. brongnartii imeonekana kuwa michanganyiko ya spishi. Spishi mpya sita zimeeleza juzijuzi.
Spishi mbili zimewekwa katika jenasi nyingine: B. simplex inaitwa Acrodontium simplex sasa na B. nivea inaitwa Tolypocladium inflatum sasa.