Kubwilu, kubwiro au naiwa ni ndege wa familia Oriolidae. Wanatokea Afrika, Asia, Australia na Ulaya. Spishi nyingi zina rangi za manjano na nyeusi, lakini nyingine zina rangi za majani, nyekundu au kahawa pamoja na nyeusi. Ndege hawa wana sauti tamu bainifu. Hula matunda, beri na arithropodi. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe kilichofuma na hili limening'inizwa kutoka tawi kama susu. Jike huyataga mayai 2-3, hata hadi 6.