Nyoka meno-hanjari ni spishi ya nyoka wa jenasi Xyelodontophis katika familia Colubridae. Amepewa jina hili kwa sababu ana chonge ndefu zinazofanana na hanjari.
Nyoka huyu ni warefu kiasi: m 1-1.5. Rangi yake ya juu ni kijivu au kahawia pamoja na vidoa njano. Taya la chini ni jeupe, koo njano na tumbo jeusi.
Makazi na mwenendo haijulikani vizuri lakini sampuli moja ilipatikana yenye kinyonga ndani ya tumbo lake.
Chonge ni meno marefu ya nyuma yanayofanana na hanjari. Haijulikani kama sumu ni hatari.