Mfenesi (jina la kisayansi Artocarpus heterophyllus; kwa Kiingereza Jackfruit, Jack tree n.k.) ni mti wa familia Moraceae.
Tunda lake huitwa fenesi na ni tunda la mti lililo kubwa kabisa kuliko matunda ya mti yote (hadi kg 36 na sm 90x20). Hata hivyo, mti mmoja unaweza kuzaa matunda 100 hadi 200 kwa mwaka.
Mbao za mti huo ni nzuri kwa utengenezaji wa fenicha mbalimbali.
Asili ya mti huu ni Uhindi. Siku hizi hupandwa mahali pengi pa kanda ya tropiki ambapo kunanyesha kiasi.