dcsimg

Mnazi (mti) ( Swahili )

provided by wikipedia emerging languages

Mnazi (Cocos nucifera) ni kati ya miti muhimu zaidi kwa ajili ya uchumi wa kibinadamu katika nchi za tropiki.

  • tunda lake laitwa nazi ni chakula
  • nyama ya tunda hukaushwa kuwa nguta (au: mbata). Nguta hutumiwa viwandani kwa kutengeneza mafuta ya kulika.
  • utomvu ni kinywaji chenye afya kwa sababu ya vitamini yake
  • utomvu uliochachuka "mnazi" ni kinywaji cha pombe
  • ubao unatumiwa kwa ujenzi wa nyumba au jahazi
  • majani kwa paa za nyumba, mikeka au makofia.
  • Mafuu ya mbegu hutumiwa kama kuni au kutengeneza vifaa vya muziki au urembo kama vile bandili, hereni au mikufu.

Mnazi ni mmea wa familia ya Palmae (au: Arecaceae). Asili yake inafikiriwa iko Asia ya kusini lakini umesambaa tangu karne nyingi sana. Mbegu wake unaweza kuzaa hata baada ya kukaa kwenye maji ya bahari kwa muda fulani hivyo inawezekana ya kwamba mnazi ulisambaa peke yake kwenye pwani za bahari. Lakini bila shaka watu waliibeba safarini kwa sababu ni chakula.

Viungo vya Nje

license
cc-by-sa-3.0
copyright
Waandishi wa Wikipedia na wahariri

Mnazi (mti): Brief Summary ( Swahili )

provided by wikipedia emerging languages

Mnazi (Cocos nucifera) ni kati ya miti muhimu zaidi kwa ajili ya uchumi wa kibinadamu katika nchi za tropiki.

tunda lake laitwa nazi ni chakula nyama ya tunda hukaushwa kuwa nguta (au: mbata). Nguta hutumiwa viwandani kwa kutengeneza mafuta ya kulika. utomvu ni kinywaji chenye afya kwa sababu ya vitamini yake utomvu uliochachuka "mnazi" ni kinywaji cha pombe ubao unatumiwa kwa ujenzi wa nyumba au jahazi majani kwa paa za nyumba, mikeka au makofia. Mafuu ya mbegu hutumiwa kama kuni au kutengeneza vifaa vya muziki au urembo kama vile bandili, hereni au mikufu.

Mnazi ni mmea wa familia ya Palmae (au: Arecaceae). Asili yake inafikiriwa iko Asia ya kusini lakini umesambaa tangu karne nyingi sana. Mbegu wake unaweza kuzaa hata baada ya kukaa kwenye maji ya bahari kwa muda fulani hivyo inawezekana ya kwamba mnazi ulisambaa peke yake kwenye pwani za bahari. Lakini bila shaka watu waliibeba safarini kwa sababu ni chakula.

 src=

Mnazi

 src=

Mnazi inavyokua katika nyumba ya kioo kwenye nchi ya Ulaya

 src=

Picha ya mnazi na tunda lake la nazi

 src=

picha ya maua ya mnazi

 src=

Nazi bila kozi lake

license
cc-by-sa-3.0
copyright
Waandishi wa Wikipedia na wahariri