Majongoo ni aina za arithropodi wembamba na warefu katika ngeli Diplopoda ya nusufaila Myriapoda wenye miguu mingi. Wanafanana kijuujuu na tandu lakini hawa huenda mbio na hula wanyama wengine (invertebrati na vertebrati). Majongoo huenda polepole na hula dutu ya viumbehai, viani na kuvu. Hata kama majongoo huitwa millipedes (miguu elfu) kwa Kiingereza na tandu huitwa centipedes (miguu mia), kwa ukweli wana kwa kadiri nambari sawa ya miguu: tandu wana miguu 16 hadi 300 na majongoo 36 hadi 750.