Mitumbaku (pia mitumbako; kwa Kisayansi Nicotiana spp.) ni mimea iliyo na asili yao katika Amerika lakini inayolimwa kote duniani sikuhizi. Majani yake (tumbaku) yana kiasi kikubwa cha nikotini na yana matumizi ya kuvuta katika sigara.
Waindio ambao ni wenyeji asilia wa Amerika walitumia tumbaku miaka mingi kabla ya kufika kwa Wazungu huko. Wahispania walijifunza matumizi ya tumbaku kutoka kwao wakaileta Ulaya.
Mwanzoni tumbaku ilivutwa kwa kiko. Sigara zilipatikana baadaye. Inatafuniwa na kunuswa pia.
Mitumbaku (pia mitumbako; kwa Kisayansi Nicotiana spp.) ni mimea iliyo na asili yao katika Amerika lakini inayolimwa kote duniani sikuhizi. Majani yake (tumbaku) yana kiasi kikubwa cha nikotini na yana matumizi ya kuvuta katika sigara.
Majani ya tumbaku yakikauka