Chande ni arithropodi wa oda Opiliones katika ngeli Arachnida wafananao na buibui. Kama hao chande wana miguu minane, lakini miguu yao ni mirefu sana katika spishi nyingi. Jozi ya pili ni mirefu kuliko mingine na hutumika kama vipapasio. Sehemu zote za mwili wao zimeungana, kwa hivyo hakuna finyo kati ya kefalotoraksi na fumbatio kama kwa buibui, lakini kama hao wana kelisera (chelicera) na pedipalpi. Hawawezi kusokota nyuzi za hariri, kwa hivyo hawatengenezi utando. Wana macho mawili tu (buibui wana 6 au 8).
Spishi nyingi hula vitu vingi (omnivores): wadudu wadogo, dutu ya mimea, kuvu, mizoga midogo na mavi. Chande wawindaji wengi huvizia mawingo, lakini wengine huwinda wakikimbia.