Tiripsi au vithiripi ni wadudu wadogo sana wa oda Thysanoptera (thysanos = nyoya yabisi, ptera = mabawa) katika nusungeli Pterygota (wenye mabawa). Wanatokea kila mahali pa dunia isipokuwa Antakitiki. Wadudu hawa ni wadogo kabisa. Spishi nyingi ni mm 1 tu au ndogo zaidi na hula kuvu na spora zao (aina za vijimbegu vya kuvu) au hufyonza maji ya seli za mimea. Spishi nyingine hula wadudu wadogo wengine na zinafika zaidi ya mm 1, lakini spishi za jenasi Idolothrips, zinazokula spora za kuvu, ni kubwa kuliko zote na zinaweza kufika mm 14. Kwa sababu ya ukubwa wao mdogo tiripsi wana mabawa sahili: umbo wa mrija bila vena wenye matamvua ya manyoya. Mandibulo ya kulia imepungua mpaka kubaki kama salio tu au imetoweka kabisa. Ile ya kushoto imekuwa sindano ya kupenya tishu ya mmea au mdudu. Koromeo iingizwa ili kufyonza maji ya seli. Kwa sababu ya hii tiripsi ni wasumbufu wakiwa wengi juu ya mimea iliyopandwa shambani.