Samaki ni wanyama wenye damu baridi wanaoishi kwenye maji ya mito, mabwawa, maziwa au bahari.
Wote ni vertebrata, yaani huwa na uti wa mgongo.
Wanatumia oksijeni iliyomo ndani ya maji kwa kuyavuta kwenye mashavu yao.
Kuna aina nyingi za samaki wadogo wenye urefu wa sentimita moja na wakubwa wenye urefu hadi mita 15. Ila tu viumbe wakubwa kwenye maji si samaki bali nyangumi ambao ni mamalia.
Samaki ni chakula bora kwa sababu nyama yake ina protini nyingi inayopokewa kwa urahisi na mwili wa binadamu. Leo hii ni zaidi ya watu bilioni moja wanaotegemea samaki hasa kama chanzo cha protini.
Tangu zamani samaki walivuliwa na watu. Wanaoishi karibu na bahari au mito mikubwa mara nyingi ni wavuvi.
Mbali na kuvua tu, watu wanafuga samaki pia. Ufugaji samaki hutokea hasa katika mabwawa madogo; samaki wanapewa lishe ili wale na baada ya kufikia ukubwa unaotakiwa maji yanaondolewa kwenye bwawa. Lakini miaka ya nyuma ufugaji samaki umeenea hadi baharini. Vizimbi vikubwa vinatengenezwa kwa seng'enge na kuzamishwa katika sehemu ya bahari pasipo hatari ya mawimbi makali kwa mfano katika hori nyembamba kama fyord za Norwei.
Samaki wanafugwa pia kama mapambo na kwa burudani: watu wanajua wale wenye rangi za pekee na kuwafuga hasa.
Hapa tunapaswa kutaja kuwa karibu na samaki ambao hutegwa na watu kwa lengo la kula, kuna uvuvi wa michezo ambayo huenea duniani kote. Kuna njia mbili: