Kwa nyota angalia hapa Chura (nyota)
Vyura ni wanyama wa ngeli Amphibia wanaoanza maisha yao ndani ya maji na baada ya kupita metamofosi wanaendelea kuishi kwenye nchi kavu, isipokuwa vyura-kucha ambao huishi majini maisha yao yote.
Maisha ya chura yanaanza kama yai lililotegwa kwenye maji pamoja na mayai maelfu. Anatoka kwa umbo la ndubwi (pia: kiluwiluwi) ambayo ni funzo ya chura anaendelea na kipindi cha kwanza cha maisha yake katika maji. Anapumua kwa yavuyavu na mwanzoni hana miguu bali mapezi kama samaki na mkia. Viluwiluwi wengi wakiwa kwenye maji wanakula majani au mwani hata kama baadaye kama chura mzima wanakula wanyama wengine.
Baada ya muda kiluwiluwi anakuza miguu minne na mapafu. Utumbo unabadilika na kujiandaa kwa chakula kipya kinachopatikana kwenye nchi kavu. Umbo linazidi kufanana na chura mzima.
Kipindi hiki cha utoto kwenye maji kinadumu kati ya wiki tatu hadi miaka miwili kutegemeana na spishi za chura. Mara nyingi ni kama wiki 10 - 15.
Akitoka kwenye maji chakula chake ni wanyama wengine hasa wadudu. Lakini chura wakubwa wameonekana pia kula mamalia wadogo, samaki na chura wadogo zaidi. Spishi kadhaa wana ulimu wa kunata wanashika wadudu wanaopita haraka lakini wengine wanakamata windo kwa kutumia mikono yao.
Bali na maelezo haya kuna pia spishi kadhaa wanaorudi kuishi katika maji lakini wanapumua kwa mapavu na wachache sana wanaendelea kula majani. Spishi kadhaa wanaendelea kuishi kwenye miti.
Chura wenyewe wanaliwa na ndege, samaki, nyoka na mamalia. Katika nchi kadhaa watu wanakula chura, kwa mfano Ufaransa, China na Ufilipino.
Kuna takriban spishi 5,600 za chura.
Kwa nyota angalia hapa Chura (nyota)
Vyura ni wanyama wa ngeli Amphibia wanaoanza maisha yao ndani ya maji na baada ya kupita metamofosi wanaendelea kuishi kwenye nchi kavu, isipokuwa vyura-kucha ambao huishi majini maisha yao yote.